
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO KIBAHA
KATIBU Mtendaji wa Baraza la ushauri na Watumiaji Huduma za Nishati na Maji(EWURACCC), Goodluck Mmari amesema kwamba malalamiko yanoongoza kutoka kwa watumiaji katika ofisi zao bi ankra za kubambikizwa ni maji na umeme.Kauli hiyo ilitolewa na Mmari katika viwanja vya Mwendapole wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya kitaifa ya 22 ya wiki ya maji yanayoendelea wilaya Kibaha." Malalamiko mengi yanayoongoza ambayo tunaletewa na ankra za kubambikizwa ambazo hazilingani na matumzi. hivyo ninapenda kuwashauri wannachi kwamba wawasiliane na mamlaka husika kwa kutumia mfumo wa sheria," alisema Mmari. Mmari aliongeza kwamba mamlaka inayohusika iatakiwa kutoa majibu kwa siku 21 hivyo kama mtumiaji hakuridhika aende katika ofisi hizo. Alisema watumiaji wengi wa huduma za nishati na maji pia hulalamikia muda mrefu wa kuunganishiwa huduma hizo.
.jpg)





0 comments:
Post a Comment