Waziri wa Kigeni wa Marekani azuru Uarabuni!

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani ,Hilary Clinton, yuko ziarani katika nchi za Ghuba, akitafuta uungwaji mkono wa Waarabu kwa ajili ya kuiwekea vikwazo vikali Iran, juu ya mpango wake wa nuclear.
Akiwa nchini Qatar, Bi Clinton atahutubia mkutano wa kimataifa kati ya Marekani na Waislamu.
Bi Clinton anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu wa Uturuki , Recep Tayip Erdogan, ambaye nchi yake inapinga vikwazo hivyo.
Baada ya hapo Bi Clinton atazuru Saudi Arabia.
Marekani inatarajia kuwa Saudi Arabia, ambayo ina uhusiano mkubwa unaozidi kukua na Uchina, itaweza kuishawishi utawala wa Beijing kuweka kando hatua yake ya kupinga Iran iwekewe vikwazo vikali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment