Rais Jakaya Kikwete akisoma hotuba yake aliowaandalia wananchi katika uzinduzi wa kampeni ya Zinduka yenye lengo la kupambana na Malaria nchini huku ikihusisha tamasha kubwa la muziki lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, ambapo wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya Bongoflreva walifanya maonyesho na kuimba nyimbo zenye ujumbe unaohamasisha jamii kupambana na kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini.
Matamasha haya yataendelea katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini ili kuelimisha na kuhamasisha umma kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Maralia.
Wakati huohuo katika hotuba yake Rais amesema ameshasikiliza kilio cha wasanii wa muziki na filamu kwa kuwanululia mtambo wa Mastaring kwa ajili ya kudhibiti uizi wa kazi za wasanii unaofanya na wanajanja wachache wenye tamaa hapa nchini, ameongeza kuwa ameshawalipia pia pango la nyumba kinachosubiriwa ni kufungwa kwamtambo huo lili uweze kuzinduliwa haraka iwezekanavyo.
Mabalozi mbalimbali wa mapambano dhidi maralia ambao ni wanamuziki wakiwa katika picha uya pamoja na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya Zinduka yenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria nchini kote.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa makampuni, Taasisi na viongozi wa serikali yanayopambana na ugonjwa wa Malaria.
Afisa habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Catherine Sungura kulia na mdau Hassan Said nao walishindwa kutulia kwenye viti vyao ikabidi wazinduke kwa kupunga mikono yao.
Vijana wa kazi B. Band wakiwa kazini hebu wacheki mwenyewe mdau nisikuchoshe kwa maneno mengi.
Mh Ray C. Jamani hapa ilikuwa kiuno bila mfupa naamini hata mbu asingekaa kutokana na kelele za mashabiki hivyo na yeye alizinduka vilivyo.
Binti Komando Lady Jay Dee naye akafanya mambo makubwa na kundi lake la Machozi Band.
Mwanamuziki Profesor J. Joseph Haule alifanikiwa kumkuna Mh. jakaya Kikwete kwa mashairi yake mazuri juu ya kampeni ya Malaria kiasi kwamba alikuwa akifurahia kila alipokuwa akiimba jukwaani.
Mh Temba kushoto na Chegge kutoka TMK Family Kimumeni wakikamua jukwaani.
Mashabiki mbalimbali wakizinduka dhidi ya malaria wakati wasanii walipokuwa wakikamua jukwaani.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Mwamvita Makamba wa pili kutoka kulia akiwa na wadau wengine wa mapambano dhidi ya Maralia Sofia Byanaku kulia na Mange Kimambi Kushoto.
Rais Jakaya Kikwete kulia akiwa anasikiliza nyimbo za wasanii kabla ya kuzindua rasmi kampeni hiyo kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete na katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa.
Mgeni rasmi Rais Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa wakati alipowasili kwenye viwanja vya Leaders ili kuzindua kampeni ya Zinduka maalum kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Mdau Bahati na wenzake kutoka JWT nao wakazinduka kwa kushikilia vyandarua vyao na kujimwayamwaya mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.
Waimbaji wa muziki wa injili Mr. & Mrs. Mbasha kushoto wakipozi kwa picha na mwanamuziki mwenzao Marlow.
Mdau Mange Kimambi katikati akipozi kwa picha na vimwana wanamitindo wa Tanzania Model Group nao waliwakilisha vyema na kuzinduka dhidi ya malaria.
Michapo ikiendelea kushoto ni Meneja udhamini na mwasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza katikati Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na kulia Naibu Mkurugenzi wa Shirika la PSI Mheshimiwa Romanus Mtung'e.
0 comments:
Post a Comment