Ni kweli kwamba baada ya uvumi kuenea kuwa katika maeneo ya Salender Bridge kuna mwanamke ambaye mkono wake uligeuka na kuota manyoya ya paka mara baada ya kumpa msaada Ombaomba, hali hiyo sasa imewawia vigumu sana wtoto mbalimbali wa mitaani ambao huishi kwa kuomba katika maeneo mbalimbali jijini.
Kama unavyoona hii picha hapa ni maeneo ya PPF Tower Posta watoto hawa walikutwa wakiwa wamelala majira ya saa 5:00 asubuhi huku wakionekana kuchoka pengine kutokana na njaa, kwa kawaida huwa siyo rahisi kuwakuta watoto hawa wamelala mapema namna hiyo huenda waliamua kulala baada ya kuona kila mpita njia wanayemuomba fedha hawapi kwa kuongopa kuwa huenda anaweza kudhurika.
0 comments:
Post a Comment