MIRIAM GERALD APANDA TENA KIZIMBANI LEO!!


Miss Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’, leo wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 na watuhumiwa hao wanaendelea kupeta kwa dhamana.Kenny na Miriam walitinga mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi, wakiwa katika gari moja aina ya Harrier yenye namba za usajili T 178 BDV na baada ya kuingia walianza kushangiliwa na mahabusu waliokuwa wakifika mahakamani hapo wakiwa katika mabasi ya Magereza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment