Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
DAR ES SALAAM IJUMAA FEBRUALI 12, 2010. Watu watano wakiwemo askari wawili wa Kampuni binafsi ya Ulinzi ya Triple D ya Jijini Da es Salaam, wanashikiliwa na Polisi mkoani Temeke kwa tuhuma za wizi wa silaha aina ya Shot Gun ikiwa na risasi tatu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi (ACP) Ribelatus Sabas, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Denis Cosmas(35) na Richard Edward(49) ambao ni walinzi wa kampuni hiyo waliokuwa zamu ya lindo kwenye kituo cha mafuta Gapco.
Amewataja wengine wanaoshikiliwa kuwa ni Patrick Asangalwisye(35), Michael Dismas(30) na mwana dada Witnes Enock(20) ambao wote ni wauzaji mafta katika Kituo cha Mafuta cha Gapco kilichopo mkabala na Uwanja wa Taifa wa zamani kwa sasa Uhuru.
Kamanda Sabas amesema kuwa tukio la kuibwa kwa silaha hiyo limetokea leo Februari 12, 2010 majira ya saa 1.30 asubuhi ambapo mlinzi wa zamu aitwaye Denis Cosmas alidai kuiacha kwenye kibanda cha ulinzi na kwenda kujisaidia na aliporudi hakuikuta.
Ametaja namba za silaha hiyo kuwa ni HB 24963A na kwamba bado Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kubaini kama silaha hiyo iliibwa nyakati za usiku akiwa amelala lindoni ama wakati alipokwenda kujisaidia.

0 comments:
Post a Comment