Mshiriki wa Bigbrother Revolution mwaka 2009 Elizabert Gupta ameingia kwenye anga za filamu baada ya kushiriki kwenye filamu ya kibongo inayokwenda kwa jina la "Danger Zone" ambayo imeshirikisha mastaa wengi wakiwemo Johari na wengine kwa sasa imekamilika katika kila hatua.
Gupta amesema katika filamu hiyo amecheza kama mke wa Raymond Kigosi aka Ray anayeitwa Nandi, ambapo maudhui ya filamu hiyo ni migongano ya familia moja yenye ndugu wawili Ray na Hemed wanaojaribu kugombea mali baada ya wazazi wao kufa.
Katika filamu hiyo Ray na ndugu yake Hemed wanagombea mali kiasi kwamba wanashindwa kuelewana kabisa kitu ambacho kinapelekea kumshawishi Ray amuue ndugu yake Hemed, na baada ya mauaji hayo anatafutwa mtuhumiwa, lakini Ray anaharibu ushahidi na kukimbia mji wake.
Baada ya kukimbia hatimaye watu wa usalama wanamkamata mke wake ambaye ni Nandi (ELizabert Gupta) na kumuweka rumande kwa muda mrefu na kuteswa sana upelelezi unafanyika , baada ya muda mrefu inathibitika kuwa Raymond Kigosi (Ray) ndiye aliyemuua mdogo wake hemed kisha anatafutwa sana na kukamatwa, anafunguliwa mashitaka na kuhukumiwa kifungo cha maisha huku mke wake Nandi akiachiwa huru
Elizabert anasema katika filamu hiyo ameonyesha uwezo wake katika kucheza filamu na mashabiki wote wa filamu wajaribu kuinunua hiyo filamu ya Danger Zone ambayo kwa sasa inapatikana katika maduka maduka mbalimbali ya filamu hapa nchini ili waone uwezo wake anaongeza kuwa ana imani kuwa wataipenda na kuifurahia
0 comments:
Post a Comment