Bi.Neema Robert mkazi wa Chang'ombe Temeke akihojiwa na waandishi wa habari.Baadhi ya walemavu wa viungo jijini Dar-es-Salaam wamelalamikia habari zilizovumishwa katika vyombo vya habari zikidai ombaomba wa Salender Bridge amemfanya mtu kugeuka mkono wake na kuwa na manyoya mithiri ya paka.
Wamesema kitendo hicho kimewafanya kunyanyapaliwa kila mahali katika sehemu mbali mbali za huduma za kijamii,wakielezea zaidi mbele ya waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, walemavu hao wamesema hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari(Radio) na magazeti vilitoa taarifa kuwa katika maeneo ya salender bridge kuna mwanamke ambaye mkono wake uliota manyoya baada ya kutoa msaada kwa omba omba waliokuwa mahali pale.
Taarifa hizi kwa mujibu wa watu mbali mbali na vyombo mbali mbali zimeonekana kuvuta hisia za watu wengi,tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo inadaiwa mwanamke mmoja alilazimika kumbusu omba omba ili arudi katika hali yake ya kawaida,kitendo ambacho kilipelekea omba omba huyo kupotea na mwanamke huyo kimazingara.
walemavu hao wamesema walifika eneo la tukio na kukitaka chombo hicho kudhibitisha taarifa hizo lakini bado haikuthibitishwa kama kuna ukweli wowote,baada ya hapo waliamua kwenda katika Idara ya habari maelezo na kutoa tamko la kuwa taarifa si sahihi na kwamba zimewafanya walemavu wa viungo na omba omba kuitwa MIZIMU na jamii nzima,pamoja na kunyanyapaliwa hata kwenye vyombo vya usafiri,migahawani na sehemu mbali mbali za huduma ya jamii.
Akihitimisha Bi.Rehema ambaye ni mmoja wa walemavu hao amesema,mpaka sasa tayari kuna walemavu 3 anaowafahamu ambao wamepewa NOTICE za kuondoka kwenye nyumba walizopanga.Hivyo wameiomba Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijaribu kuliangalia swala hilo kwani maisha yao hivi sasa yamekuwa ni yenye huzuni na masikitiko na wakati mwingine kujiona hawafai kuishi.

0 comments:
Post a Comment