Mauritania yamuita balozi wake wa Mali

Mauritania iemuita nyumbani balozi wake wa Mali, baada ya serikali ya Mali kuwaachilia huru wanachama wanne wa mtandao wa kundi la Al Qaeda.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mauritania, imesema hatua hiyo inakiuka makubaliano ya kiusalama yaliyofikiwa baina ya nchi hizo mbili jirani.
Jana Mali iliwaachilia huru wapiganaji hao, mmoja akiwa raia wa Mauritania, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mpango wa kuachiliwa mateka wa Kifaransa.
Kundi la Al Qaeda katika nchi za Maghreb, lilidai wapiganaji wake waachiliwe huru kwa kubadilishana na mateka huyo, Pierre Camatte.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment