Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe amemteua Rosemary Lulabuka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) .
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotelewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Hamis Dihenga inasema kuwa uteuzi huo ulianza February Mosi mwaka huu.
Alisema kuwa Waziri Maghembe amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Elimu Tanzania namba 8 ya mwaka 2001 ilianzisha Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Dihenga alisema kuwa kabla ya uteuzi huo, Lulabuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Mei, 2009 na pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Mamlaka hiyo.
Aliongeza kuwa Lulabuka amewahi pia kufanya kazi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akiwa Mhasibu Mwandamizi.
Dilenga alisema kuwa Lulabuka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bibi Mercy Silla aliyeteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru tangu Aprili, 2009.
Bibi Lulabuka ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara(Master Degree in Business Administration ) na Certificate Public Accountant (CPA-T).

0 comments:
Post a Comment