TANGANYIKA LAW SOCIETY KUFANYA MKUTANO WA MWAKA ARUSHA!!

Dr. Fauz Twaib Rais wa Tanganyika Law Sociaty akizungumza na wandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo wakati akizungumzia mkutano wa mwaka wa Taasisi hiyo ya kisheria utakaofanyika jijini Arusha februari 19/2010 katika ukumbi wa mikutano wa AICC na kuhusisha wanasheria mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Zimbabwe.
Mambo yatakayoongelewa nia pamoja na masuala mazima ya Demokrasia na utawala wa sheria, mambo ya haki za wanawake, pia yatazungumziwa mambo yahusuyo Zanzibar na suala la Mgombea Binafsi, wasomi na wanasheria kutoka mataifa mbalimbali watawasilisha mada zao.
Mkutano huo mkubwa unatarajiwa kufunguliwa na Mh.Mizengo Pinda waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment