Wachezaji wa Simba na Zesco wakichuana vikali wakati wa pambano lao la kujipima nguvu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar leo.
Mashabiki mbalimbali wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakiangalia pambano hilo.
Timu ya Simba ya jijini Dar leo imetoka kifua mbele katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam baada ya kuifunga timu ya ZESCO kutoka nchini Zambia magoli 4-1 katika mchezo wa kirafiki uliokuwa mkali wakati wote.
Simba ikicheza kwa kujiamini iliweza kupata magoli mawili kupitia kwa wachezaji wake Nico Nyagawa na Make Barasa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo huku kila upande ukionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo.
Katika kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani zikitafuta magoli, hata hivyo walikuwa simba tena walioliandama lango la ZESCO na kuongeza magoli mengine mawili kupitia kwa mchezaji wake yuleyule Mike Barasa ambaye alionekana kuwa mwiba mkali kwenye ngome ya timu hiyo ya Zambia
ZESCO walijitutumua na kupata goli moja kwenye kipindi cha pili lililofungwa na mchezaji wao Enock Kasala hivyo kufanya timu hizo kutoka nje zikiwa Simba 4-Zesco 1 mara baada ya mpira kumalizika.
Wakati huohuo taarifa kutoka kwa msemaji wa timu ya Yanga Louis Sendeu zinasema Timu hiyo imefurushwa mbali katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufungwa goli moja na timu ya FC Lupopo katika mchezo uliochezwa katika jimbo la Katanga nchini DRC goli lilifungwa na mabeki wa Yanga baada ya kubabatizwa na washambuliaji wa FC Lupopo katika Dakika ya 89 ya mchezo hivyo Yanga imetolewa kwa magoli 4-2
1 comments:
Aisee kumbe Bukuku ni Simba damu
mdau
kisiju pwani
Post a Comment