EU yakasirishwa na marufuku ya Libya!

Rais Muamar Gadaffi wa Libya.

Tume ya bara Ulaya imeshtumu uamuzi wa Libya wa kusitisha kutoa viza kwa raia wa bara Ulaya ambao wanaruhusiwa kwenda nchi moja hadi nyengine bila kizuizi.
Tume hiyo inasema "imesikitishwa na uamuzi huo usiyo mzuri" wa Libya na nchi zilizo katika mpango wa Schengen zitatafakari "hatua watakayochukua".
Libya ilichukua hatua hiyo baada ya Uswisi kudaiwa kuwanyima ruhusa ya kuingia kwao viongozi 188 wa Libya.
Marufuku ya Uswisi inasemekana kujumuisha kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na jamii yake.
Uswisi ni moja kati ya nchi 25 zilizoko kwenye eneo la Schengen -nchi za bara ulaya zilizoondowa masharti ya kupita kwenye mipaka yao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment