BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music band imewanyakuwa waimbaji, Hamisi Tenguweni'Super Maliki' akitokea bendi ya Makoba Band ambapo amewahi kuimbia bendi ya TOT plas na Shikamoo Jazz zote za jijini Dar es salaam pamoja na Mohamedi Mwerevu 'Muddy Clever' akitokea bendi ya Maruni Komando,ambaye pia amewahi kuimba katika bendi za Nyota Sound Afrika na Lessi Wanyika zote za Kenya
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa kundi hilo, Rajabu Mhamila 'Super D'Alisema, wameamua kuwachukuwa waimbaji hao kwa kuwa wana uwezo wa kuisaidia bendi na sasa wameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo mpaka sasa wanajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka huu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yao ya "Huna shukrani" ambayo inauzwa mtaani katika maduka mbalimbali.
Wakati huohuo, bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi inakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapili wapo jijini Dar es Salaam huku wakiwa tayari na nyimbo mbili mpya moja ni "Lipi jema" uliotungwa na Eddo Sanga na "Dawa ya Deni" kulipa wa Isihaka Katima 'DJ Papa upanga'
Amesema, sambamba na burudani hizo pia wamejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka huu mapema kadiri iwezekanavyo alisema Mhamila,
Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhuria kwa wingi ili kuona maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo hazihitaji kuhadithiwa





0 comments:
Post a Comment