Shirika moja la kutetea haki za binadamu huko Nigeria limewasihi wabunge wa nchi hiyo kumtangaza Rais Umaru Yar'Adua kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza kutokana na hali yake ya afya.
Shirika la waandishi wa haki za binadamu pia limelitaka bunge kutuma ujumbe kwenda kumsaka Rais huyo.
Majaji pia wanatarajiwa kusikiliza kesi mbili tofauti zilizofikishwa mahakamani juu ya Rais Yar'Adua kutokuwepo kwa muda mrefu madarakani.
Ameshindwa kukabidhi madaraka kwa naibu wake na hivyo Wanigeria wengi wanaona kwamba kuna ombwe ya uongozi nchini humo.
Wakili na mwanaharakati Femi Falana, amewataka majaji kufuta maamuzi yote yaliyofanywa na bunge bila ya Rais huyo kuwepo.

story by http://www.bbcswahili.com/
0 comments:
Post a Comment