SIMBA YAITUNGUA TIMU YA PRISON KWENYE UWAJA WA UHURU!!

Kutoka kushoto ni kocha wa timu ya Simba Patrick Phiri, Meneja Inocent Njovu na Amri Said kocha msaidizi wa timu hiyo wakifuatilia pambano katika ya timu yao na timu ya Prison kutoka mkoani mbeya.


Timu ya Simba ya jijini Dar es salsaam leo imeitungua timu ya magereza Prison kutoka mkoani Mbeya kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Uhuru maarufu kama (shamba la bibi).
Mchezo huo ulikuwa ni mkali lakini kama kawaida yake timu ya Simba ilionekana kutawala karibu kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo na kufanya mashambulizi mengi katika lango la timu ya Prison, hata hivyo kazi nzuri ya golikipa wa timu hiyo ndiyo iliyoiokoa Prison.
Katika kipindi hicho cha kwanza simba ilifanikiwa kupata magoli kupitia wachezaji wake Mussa Hassani "Mgosi" aliyeifungia timu hiyo goli la kwanza huku mchezaji mwingine Nico Nyagawa akifunga goli la pili.
Katika kipindi cha pili timu ya Prison ilijitutumua na kujipatia goli la kwanza na la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wake Misango Magae, goli lililoipa nguvu timu hiyo na kushambulia lango la timu ya Simba mara kwa mara bila mafanikio.
Shujaa wa simba Mussa Hassan Mgosi aliwanyanyua mashabiki wake tena mara baada ya kukandamiza goli la tatu kwenye lango la Prison goli lililoifanya timu hiyo kunyong'onyea kabisa kimchezo, hata hivyo mara baada ya mchezo huo kocha wa Prison James Nestory amesema timu yake imefungwa kimchezo kwani timu ya Simba ilicheza vizuri, lakini pia wachezaji wake hawakuwa vizuri kimchezo kutokana na kuathirika kisaikolojia kwa sababu ya kupoteza michezo mingi ya ligi kuu ya Vodacom.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment