Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa marehemeu Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo jioni Marehemu mzee Kawawa anatarajiwa kuzikwa kesho majira ya saa 7:00 mchana nyumbani kwake Kunduchi Madale.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee, jijinji Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee, jijinji Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
Viongozi wa serikali, Vyama, mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimabli pamoja na Ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika mstari kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa.
Rais Jakaya Kikwete katikati akiwa amekaa wakati dua mbalimbali zilipokuwa zikisomwa leo jioni kwenye ukumbi wa Karimjee kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Dr. Ally Mohamed Shein na kulia ni Waziri Mkuu Mh. Pinda na Mwisho kulia ni Mke wa Rais Mama Salama Kikwete wakiwa wamekaa kwa majonzi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. William Lukuvi akiwatuliza wanafamilia waliokuwa wakilia kwa uchungu mara baada ya Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa kuwasili katika viwanja vya Karimjee.
1 comments:
Pumzika kwa amani baba yetu.
Post a Comment