Mahakama moja nchini Ethiopia imewahukumu kifo watu watano na wengine 33 kutumikia kifungo cha maisha jela, kwa kupanga mauaji ya maafisa wa serikali.
Waendesha mashitaka wamesema baadhi ya waliokutwa na hatia wanatoka katika kundi la Ginbot 7, linaloongozwa na Berhanu Nega, mkosoaji wa serikali anayeishi nchini Marekani.
Bw Nega ni miongoni mwa watu waliohukumiwa kifo, pamoja na kiongozi wa upinzani Melaku Tefera.
Bw Melaku na watuhumiwa wengine 27 walikuwepo mahakamani, mjini Addis Ababa.
Baadhi ya watuhumiwa wamesema wameteswa ili wakiri makosa hayo.
Akitoa hukumu hiyo mwezi Novemba, Jaji Adem Ibrahim amesema mahakama haikuridhishwa na madai ya uteswaji.

0 comments:
Post a Comment