kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bandi kesho watafanya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani kwa sataili ambayo aijawai kufanyika nchini imefahamikaMsemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' ameiambia tovuti hii kwamba uzinduzi huo utafanyika kesho jumanne Desemba 8, katika ukumbi wao wa Amana uliopo Ilala, katika uzinduzi huo bendi ya African Star wana wa 'Twanga Pepeta' yenye mashabiki lukuki nchini watawasindikiza ndugu zao wa Msondo
Akielezea maandalizi zaidi Mhamila alisema licha ya kusindikizwa na bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo kila mpenzi atakaekata tiketi ya kuingia ukumbini atapewa zawadi ya albam yao mpya,
Alisema nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, Huna shukrani uliotungwa na Saidi Mabera,Kiapo (husein jumbe) aki yangu ipo wapi (Uluka Uvuluge) Mama Cos, uliotungwa na marehemu (Josephe Maina) Albino (Juma Katundu) Machimbo Isihaka Kitima dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo





0 comments:
Post a Comment