WHO YAMWAGA MISAADA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII!!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizungumza mbele ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati Wizara hiyo ilipokabidhiwa msaada wa magari, Pikipiki na vifaa mbalimbali na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dr. Jean Baptiste Kapko katika ofisi za wizara hiyo mtaa wa Samora leo, vifaa vilivuyokabidhiwa kwa Wizara na shirika hilo ni Magari 14 ya kubebea wagonjwa aina ya Toyota Landcruser, magari mengine 5 aina ya Toyota Pickup,Pikipiki 5, Kompyuta za mkononi , Jokofu la Kuhifadhia Damu na mashine ya Kurudufu (Photocopy Machine) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.3 sawa na dolla za Kimarekani 985,718, Shirika hilo la afya Duniani limetoa msaada huo katika wakati muafaka kutokana na matatizo mengi yanayoikwamisha sekta ya afya kutoa huduma hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali kupitia wizara yake ya Afya na Ustawi wa Jamii, kushoto kwa waziri ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Aisha Kigoda.
Waziri Mwakyusa kulia Akipokea msaada wa moja ya magari 14 ya kubebea wagonjwa aina ya Toyota Landcruser yaliyokabidhiwa kwa Wizara hiyo na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Dr Jean Baptiste Tapko katika makao makuu ya Wizara hiyo.
Waziri Mwakyusa hapa akiangalia moja ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa Wizara na Shirika la Afya Duniani (WHO) leo anayeangalia kushoto ni Naibu waziri wa wizara hiyo Aisha Kigoda.
Waziri Mwakyusa akiangalia mashine ya kurudufu (Photocopy Machine) mara baada ya kukabidhiwa leo.

Waiziri wa Afya Prof. David Mwakyusa wa sita kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea msaada huo leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment