Wazazi wilayani Kondoa watakiwa kusomesha watoto wao

Na Anna Nkinda - Maelezo, Kondoa
Wazazi wilayani Kondoa wametakiwa kuwasomesha watoto wao kwa bidii na kutilia mkazo suala la elimu kwani Ulimwengu wa sasa bila ya kuwa na elimu ya kutosha huwezi kuwa na maendeleo ya maana.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa akiongea na wakazi wa wilaya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa hivi sasa kuna umuhimu wa kusomesha watoto wote wa kike na wa kiume bila ya kuwabagua kwani hao ndio watakaokuja kuwatunza hapo baadaye wakiwa wazee.
"Ninawaomba muwahimize watoto wenu wasome kwa bidii elimu Dini na elimu Dunia kwani kama mtoto akiwa na elimu hizi zote mbili atakuwa katika maadili mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu na wanadamu", alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment