WAREMBO MISS EAST AFRIRCA KUANZA KUWASILI WIKI HII!!

Nediat (21) ETHIOPIA
Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2009 wataanza kuwasili Nchini kuanzia wiki hii tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi wa 12 katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.
Aidha, warembo watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo wanatarajiwa kutangazwa kesho kutwa baada ya kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuratibu zoezi hilo kukamilisha kazi yake.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Nchi zinazoshiriki mashindano hayo kuchagua warembo wenye viwango vya hali ya juu ili kuziwakilisha katika mashindano ya mwaka huu
Miss East Africa 2009 itashirikisha warembo kutoka katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, na Mauritius ambazo zote zimeshathibitisha ushiriki wao.
Mashindano hayo makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa makampuni yanayodhamini mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, Kings & Queens Worldwide, CMC Automobiles Limited na AKO Catering Services Ltd.

Dalysha Nirena Doorga (21) MAURITIUS

Fatma Abdulahi (20) SOMALIA

Tabitha (20) KENYA

Queen Belle Monique (23) BURUNDI

Fatma Abdulahi (20) SOMALIA

Rebecca Getachew (23) ETHIOPIA

Asli Osman Mahamud (20) –SOMALIA

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment