Tiger Woods atoka hospitalini!

Tiger Woods.

Mcheza gofu namba moja duniani Tiger Woods ametoka hospitali baada ya matibabu ya ajali ya gari Florida Marekani siku ya Ijumaa.
Taarifa za awali zilieleza alijeruhiwa vibaya, lakini baadae mtandao wake ulifahamisha "alilazwa, akatibiwa na akaruhusiwa akiwa hajambo".
Gari lake inaarifiwa liligonga bomba la maji ya kuzimia moto barabarani na baadae likauparamia mti.
Woods, aliyeshinda mashindano 14 makubwa duniani, inaelezwa amepata majeraha usoni.
Mkewe Elin aliwambia polisi ilimbidi atumie fimbo ya kuchezea gufu kuvunja kioo cha nyuma cha gari baada ya kusikia kishindo cha ajali akiwa nyumbani. na

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment