TBL YATOA MSAADA WA MILIONI 8 IYUNGA SEKONDARI!!

Mkuu wa Shule ya Sekondari Ufundi ya Iyunga,France Mng'ong'o (kulia) akitoa shukrani baada ya Ofisa Uhusiano wa Kampni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu kumkabidhi msaada wa saruji,mabati na mbao vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 8,ikiwa ni msaada wa TBL kwa ajili ya
kusaidia kuezeka vyumba vinne vya madarasa. Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo Jijini
Mbeya jana.
Ofisa Uhusiano wa Kampni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akimabidhi Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Ufundi ya Iyunga, France Mng'ong'o, msaada wa saruji, mabati na mbao vyote
vikiwa na thamani ya sh. milioni 8,ikiwa ni msaada wa TBL kwa ajili ya kusaidia kuezeka
vyumba vinne vya madarasa. Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo Jijini Mbeya jana.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. NINAIKUMBUKA SHULE YA IYUNGA ILIVYOKUWA NZURI SANA KWANI KABLA YA UHURU ILIKUWA NI YA WATOTO WA KIZUNGU TU. SHULE HII ILIKUWA NA BWAWA LA KUOGELEA, MASHINE ZA KUFULIA NA KUPIGA PASI NGUO, BAKERY YA MIKATE NA KEKI, HEATER ZA MAJI MOTO YA KUOGA KILA BWENI, HOSPITALI VIWNJA VIZURI VY AINA TOFAUTI YA MICHEZO, MAABARA NZURI ZA SAYANSI PAMOJA NA USAFI ULIOTUKUKA; HII ILIKUWA MWANZONI MWA MIAKA SITINI, ULIPOFIKA MWAKA WA SABINI SHULE ILIANZA KUHALIBIKIWA KWA KILA KITU HATA MAJENGO YALIYOKUWA YA DARAJA LA KWANZA YAKAANZA KUWA MANYANGARAKASHA. HII INAONESHA WATANZANIA TUSIVYOJALI KITU NA KUPITWA NA USTAARABU WA UTUNZAJI NA USAFI NA NDIYO KINACHOTOKEA SASA KWENYE UWANJA MPYA WA TAIFA. SIFA YA UZURI WA IYUNGA MIAKA YA SITINI ILIWAFANYA WAKAZI WA MBEYA KUIPENDA SANA.

Post a Comment