MISS EAST AFRICA RWANDA LEO SERENA HOTEL!!

Kamati ya Miss East Africa, ikiwa pamoja na Waziri wa Jumuiya ya AfrikaMashariki Rwanda, Madame Monique Mukaruliza (mwenye suti) pamoja nawarembo wanaowania shindano la Miss East Africa Rwanda. kulia kwa wazirini Bosi wa Udhamini, Matukio na Uhusiano wa New Habari (2006) Limited,Petter Mwendapole, wakati kushoto ni Rena Callist na Adam Kapama kutokaRena Events.
Wasichana wanaoshiriki shindano la Miss East Africa wakiwakatika picha ya pamoja

WASICHANA 12 leo wanatarajia kupanda jukwaani katika hoteli ya Serenamjini hapa kwa ajili ya kuwania taji la Miss East Africa Rwanda.Mshindi wa kwanza na wa pili katika shindano hilo watawakilisha Rwandakatika fainali za Miss East Africa zitakazofanyika Desemba 18 mwaka mjiniDar es Salaam.
Mshindi wa shindano la leo ataondoka na kitita cha faranga za Rwandamilioni moja sawa na karibu sh milioni tatu za kitanzania.Mshindi wa pili ataondoka na Faranga mia tano sawa na karibu milioni mojana nusu za Kitanzania.Tayari Kamati ya Miss East Africa makao makuu iko mjini hapa kwa ajili yakushuhudia shindano hilo ambapo Jaji mkuu usiku wa leo atakuwa RenaCallist, mkurugenzi wa Rena Events.Pia Miss East Africa, anayemaliza muda wake,
Claudia Niyonzima atakuwepokushuhudia shindano hili pamoja na Miss Burundi wa mwaka jana AliceKaneza.Wakati shindano hilo linashirikisha warembo hao 12, mchuano mkali zaidiunaonekana kuwahusisha warembo wanne ambao wanachuana kwa vitu vingi.Nafasi kubwa sana inaonekana kwenda kwa Sabrina kaganza, Leticiaumuizayire, Annet Mahoro na Cynthia Akazuba.Lakini pamoja na hao wanne msichana mwingine ambaye anaweza kufanyamaajabu usiku wa leo ni Viviane Umulisa.
Warembo hao juzi walikutana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wahapa, Joseph Habineza ‘Mr Joe’. Jana pia walikutana na Waziri wa AfrikaMashariki wa hapa Monique Mukaruliza.Warembo wengine ambao wanashiriki shindano hilo ni pamoja na ClariseIshimwe, Rita Uwera, Pamela Ungabire, Clarise Ushuti na SoniaUwambambazi,

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment