Mwanasoka bora Afrika wa BBC

Wachezaji watano wametajwa kugombea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anayetambuliwa na BBC mwaka 2009.
Waliotajwa ni: Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast), Michael Essien (Chelsea na Ghana), Samuel Eto'o (Inter Milan na Cameroon), Tresor Mputu Mabi (TP Mazembe na DR Congo) na Yaya Toure (Barcelona na Ivory Coast).
Ingia hapa uweze kupiga kura kwa njia ya wavuti
Namba ya kutuma ujumbe au SMS ni +447786 200 070 ( kwa wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, hii ni tofauti na namba ya kawaida).
Unaweza kumpigia kura mchezaji wa chaguo lako mpaka tarehe 4 Januari na mshindi atatangazwa siku nne baadaye, Januari 8 huko Angola wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Tuzo hiyo ya hadhi kubwa ndiyo pekee ya aina yake kutolewa kutokana na idadi ya kura zinazopigwa na mashabiki wa soka.
Mshindi wa mwaka jana alikuwa Mohamed Aboutrika wa Al Ahly na Misri, aliyeisadia nchi yake kutetea kikombe cha kombe la mataifa ya Afrika na kuiwezesha timu yake kuchukua kombe la ligi ya vilabu bingwa Afrika.
Waliowahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika2008 - Mohamed Aboutrika2007 - Emmanuel Adebayor2006 - Michael Essien2005 - Mohamed Barakat2004 - Jay-Jay Okocha2003 - Jay-Jay Okocha2002 - El Hadji Diouf2001 - Sammy Kuffour2000 - Patrick Mboma

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment