DI BANJI ANAIPENDA TANZANIA, ATAKAMUA KESHO TANGANYIKA PAKERS!!

Mwanamuziki Di Banji Kutoka Nigeria anayepiga muziki wa Dancall akizungumza na wandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika kwenye kiwanda cha Sigara TCC barabara ya Nyerere wakati alipozungumzia ziara yake nchini na onyesho analotarajiwa kulifanya kesho kwenye viwanja vya Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam Novemba 28, katika mkutano huo mwanamuziki hyo aliongozana na wanamuziki wengine ambao atashirikiana nao katika onyesho hilo ambao ni Nameless na Nonini kutoka nchini Kenya walioko katika picha ni Isamba Kasaka (Brand Castopian) kulia na Jackie Lemboko Meneja wa Matamasha kushoto
Nameless akiongea mbele ya wanahabari wakati wa mkutano ulifanyika leo kwenye kiwanda cha sigara TCC barabara ya Nyerere.
Mwanamuziki Di Banji kutoka Nigeria wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wengine kutoka nchini Kenya wa kwanza kushoto ni Nameless, anayefuatia ni Nonini, katikati ni Dr. Sid kutoka Mo Hits Records ya Nigeria na mwisho kulia ni Ikechukwau Rapa aliyeongozana na Di Banji hii ilikuwa ni baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye kiwanda cha Sigara TCC barabara ya Nyerere leo.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment