ALGERIA YAFUNGA MDOMO WA MISRI, YAKATA TIKETI YA AFRIKA KUSINI 2010!

Kikosi cha Algeria.
Goli la Algeria lililopatikana kipindi cha kwanza Dakika ya 40 limewapa ushindi wa kihistoria Algeria dhidi ya Misri usiku wa kuamkia leo katika mechi ya (play off) iliyochezwa nchini Sudan.Kwa ujumla mchezo ulikuwa ni mkali na wenye kasi sana...wallahi waarabu wana fitina sana,
Rafu na ubabe vilitawala mechi hii na kila upande wakijaribu kucheza kwa makini kuepuka kupoteza mchezo, hata hivyo algeria ndiyo wamekuwa vinara wa mchezo huo baada ya kukata rasmi tiketi ya kwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la dunia mwaka ujao 2010.
Mchezo huo ulikuwa wa marudio baada ya mshindi kutopatikana katika mchezo wa awali ulichezwa nchini Misri,
Kukiwa na ulinzi mkali kutokana na hofu iliyokuwa imetanda juu ya uwezekano wa mashabiki wa timu hizo mbili kushambuliana kutokana na uhasama wa miaka mingi, Shirikisho la mpira Afrika CAF liligawa tiketi zipatazo elfu 9000 kwa mashabiki wa soka kutoka Misri na Algeria na walikuwa wametenganishwa katika maeneo ya kukaa wakati wa mchezo huo ili kusitokee vurumai yoyote kama zilizotokea Katika mchezo wa awali nchini Misri ambapo mashabiki wapatao 30 hivi walijeruhiwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment