ZANZIBAR YA KALE NA YA SASA KATIKA VIVUTIO VYA UTALII!!

Kanisa la kwanza la Kianglikana katika ukanda wa Afrika Mashariki linalopatikana Zanzibari Pia.
Sanamu za wa Binadamu wakati wa biashara ya utumwa sanamu hizi zinapatikana Kisiwani Zanzibar.
Hawa ni nyani wekundu ambao wako hatarini kutoweka Duniani na wanapatikana katika msitu wa Taifa wa Jozani Zanzibar.

NA JONATHAN VENANCE TOSSI
DAR ES SALAAM
Je watanzania wanafaidakaje na vivutio vya utalii vilivyoko visiwani zanzibar ?
Swali hilo linajibiwa na mhifadhi wa hifadhi ya jozani visiwa alipokuwa akiwaelezea waandiwa wahabari walipotembelea hifadhi hiyo yapekee na yenyevivutio ambavyo Afrika mashalikinakati na duniani vinapatikana Zanzibar ,anasema pamoja na kuwa na hifadhi nzuri wazawa wengi bado hajaonesha kunufaika nazo .Bw shukwa shaban ally alisema nijukumu la kila mdau kusisitiza watanzania kutembelea hifadhi hizo na kuondokana na dhana ya kuwa vivutio vya kitali ni vya watu toka nje
Muongozaji wageni huyo alisema hifadhi ya jozani imejaliwa kuwa na vivutio vingi ambavyo havionekani popote duniani ila hapo hiyo ni fursa ya kila mtanzania wa bara na visiwani kutembelea .
Alibainisha kuwa hifadhi hiyo imejaliwa kuwa na kima ,chui ,mikoko na miti mbalimbali ambayo ni dawa kama mkaratusi uuwache mvule maji na mingine mingi .
Hadi sasa hifadhi hiyo imezungukwa na kima wengi wekundu ambapo imekana kuwa zaidi ya kima 2300 kwa sasa pia alibainisha kuwa kima hao wamekuwa wakikubaliana na hali ya hewa ya jozani kwani siku za karibuni wamewapeleka kima 100 ila hadi sasa waliopo hawazidi 10
“Kwakweli napenda kutumia nafasi hii kuwasii watanzania wenzangu kutembelea hifadhi zetu na kuondokana na dhana ya kuwa vivutio hivi ni kwa ajili ya wageni ,“ alisema ally .kuhusiana na kupungua kwa chui alisema hali hiyo imetokana mkakati wa serikali wa kuwauwa kutokana na dhana ya kuwa wapo baadhi watu ambao walikua wakiwatumia kwa uchawi
Alisema kutokana juhudi hizo za kuwauwa chui hao idadi yake imepungua lakini bado wamekuwa wakionekana marakwamara katika maeneo jirani na hifadhi hiyo.Aidha alisema kuwa hifadhi ya taifa ya jozani imekua ikisifika kwa kuhifadhi maji kutokana na ardhi yake jambo ambalo linachangia kuwepo kwa kijani kibichi kila mara kwa baadhi ya maeneo pia historia ya mji mkongwe wa Zanzibar bado imekua ikivuta na kupelekea watarii wengi kutembelea mji mkongwe wa zanzibar alihitimisha shaaban ally mhifadhi hifadhiya taifa jozani .

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment