
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Heri Mwawalo
NA ZAWADI MSALLA
MAELEZO-BUTIAMA
Wazazi kote nchini wameaswa kuwasomesha watoto wao ili waweze kuwasaidia wakati wa uzeeni na kuachana na tabia ya kuwanyanyasa.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Heri Mwawalo leo Kijijini Butiama wakati Mwenge huo ulipofika katika makazi ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kupokelewa na mama Maria Nyerere.
Mwawalo amesema kuwa ni wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu itakayowasaidia hata wao katika kipindi cha uzee.
" Watoto wana haki ya kuheshimiwa na kupewa elimu, bado jamii haizingatii hilo," alisema.
Lengo la kukimbiza Mwenge kitaifa kila mwaka ni kuwakumbusha na kuwaelimisha watanzania mambo mbalimbali ya kuenzi pamoja na nini kinachotakiwa kufanywa hivi sasa.
Alisema watoto wengi hasa wa vijijini bado hawapewi fursa ya elimu kama wale wa mjini na kuwanyima haki yao ya msingi.
Akizungumzia suala la ukatili wa mauaji ya albino alisema,albino wengi wanaishi katika wakati mgumu sana kwa sasa hali inayopelekea baadhi yao kuogopa kwenda shule na hivyo kuwarudisha nyuma kimaendeleo. Alisema jamii ni lazima itambue maisha yao yanathamani kama yabinadamu yeyote Yule.
0 comments:
Post a Comment