Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald ambaye ni miss Mwanza pia akipungia mashabiki wake mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kartika shindano lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City na kushirikisha warembo wapatao 29 hivi baada ya mmoja wao kutolewa katika shindano hilo kutokana na kugundulika kuwa ni mjamzito.
Mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili umetoa mrembo wa Tanzania na kudhihirisha uwezo wake katika mashindano hayo makubwa na yenye mvuto nchini, Miriam anachukua nafasi ya Vodaciom Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim ambaye pia alitokea mkoani mwanza na kuufanya mkoa huo kuzichachafya kanada za Mkoa wa Dar es salaam Ilala Temeke na Kinondoni ambazo mara nyingi zimekuwa zikijitapa kuwa ndizo zenye warembo bomba kitu ambacho kimedhihirisha kuwa Tamb zao ni hazimzuii tembo kutoka Mwanza kunywa maji kisimani.
Miriam Gerald FULLSHANGWE inakutakia kila mafanikio katika kazi zako zote za Miss Tanzania ni kazi ngumu lakini ukiwa makini, ukajiheshimu na kusikiliza ushauri utashinda majaribu yoyote katika kazi hizo Mungu akujalie sana
Vodacom Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald akiwa katika gari yake aina ya Suzuki Grand Vitara mara baada ya kukabidhiwa baada ya kushinda taji hilo,
Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwa katika picha ya pamoja na washindi wengine mara baada ya majaji kutangaza washindi kwenye shindano lililofanyika usiku wa leo kwenye ukumbi wa Mlimani City kulia ni Beatrice Lukindo mshindi wa pili na kushoto ni Julieth miki mshindi wa tatu.
Mrembo miriam Gerald akishangilia mara baada ya kuibuka mshindi wa taji la Vodacom Miss Tanzania katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.
Mewa Bodi ya Utalii nchini Geofrey Meena akmvisha taji la Ubalozi wa Utalii nchini mrembo Sia Ndeskoi
Naibu Mkurugezi wa Utafiti na Mafunzo Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa akitangaza mshindi aliyejinyakulia taji la Utalii lililotolewa na Bodi ya Utalii nchini TTB kulia Meneja Masoko wa bodi hiyo Geafrey Meena akishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya Bia TBL David Minja akimkabidhi zawadi yake mrembo Miriam Gerald mara baada ya kutangazwa kuwa Redds Miss Photogenic jana. kulia ni meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo akishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya majaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel katikati wakijumulisha matokea ya mwisho ili kumpata mrembo wa Vodacom Miss Tanzania kazi iliyofanywa kwa ufasaha na umakini.
Hapa baadhi ya warembo wakipita na vazi la jioni.
Baadhi warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni
Naye Ray C. akamwaga uno na kulizungusha kama pia kama ilivyo kawaida yake.
Vijana hawa kutoka Nchini Uganda nao walifanya mambo makubwa kutokana na uwezo walionao katika kuimba na kutawala jukwaa,mara nyingi wanamuziki kutoka uganda wamekuwa na uwezo mkubwa katika muziki ukilinganisha na wanamuziki wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki.
THT kama kawaida ya wakafanya makamuzi makubwa jukwaani hili ni kundi la kuigwa kwakweli wadau.
Mdau Muddy kushoto na rafiki yake pia hawakutaka kukosa kinyang'anyiro hicho pale mlimani City.
Mboni Masimba kushoto na rafiki yake Joan na rafiki yao wakitaka kujua
mambo yanavyokwenda
mambo yanavyokwenda
Jokate Mwegelo kushoto akiwa na rafiki zake Natalie na Elsi.
Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akiwa na Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Lager George Kavishe.
Mdau wa Simba Nick Butt na maiwaifu wake kulia na Mdau Rodrick Mwambene aliyekaa nyuma na maiwaifu wake kushoto wakipozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.
Mgeni Rasmi katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ladislaus Komba kulia, Ibrahim Mussa Naibu Mkurugenzi wa Utafiti na mafunzo Bodi ya Utalii na aliyekuwa mkurugenzi wa Africa Media Group Franco Tramontana wakifuatilia kwa karibu wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea jana.
1 comments:
hao THT wamezidi kuiga sana, hawana viyu vyao wenyewe?
Post a Comment