Hajati Amina Mrisho Said Mkuu wa Moa wa Pwani
Na Anna Nkinda – Maelezo, Kibaha
04/10/2009 Jumla ya wanafunzi 287 wamepata ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa katika mkoa wa Pwani na hivyo kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari.
Na Anna Nkinda – Maelezo, Kibaha
04/10/2009 Jumla ya wanafunzi 287 wamepata ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa katika mkoa wa Pwani na hivyo kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa huo Hajati Amina Mrisho Said wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyetembelea shule ya Sekondari Magindu iliyopo wilayani Kibaha kwa ajili ya kutoa msaada wa magodoro 100 na vitanda vitanda vyake.Hajati Amina alisema kuwa wilaya ya Rufiji inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata ujauzito kwani kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 130 wamepata ujauzito ambapo wanafunzi wa Shule ya Msingi ni 110 na Sekondari ni 20.Aliitaja wilaya ya Mafya kuwa haina tatizo kubwa la wanafunzi kupata ujauzito ukilinganisha na wilaya zingine kwani kwa mwaka huu waaunzi wa shule ya Msingi watatu na sekondari kumi ndio waliopata uajauzito.
0 comments:
Post a Comment