SIA NDASKOI MISS DOMESTIC TOURISM 2009 ALAMBA ZAWADI ZAKE KUTOKA TTB!!

Miss Domestic Tourism Sia Ndaskoi ambaye ndiyo balozi wa Utalii nchini akipozi kwa picha mbele ya Camera ya FULLSHANGWE mara baada ya kupokea zawadi zake leo kutoka Bodi ya Utalii nchini, ambapo alikabidhiwa kompyuta yake yenye thamani ya shilingi milioni 1.1 na cheki yenye thamani ya shilingi milioni 2.2, Sia ameaswa kuwa makini na kazi yake kama balozi wa utalii nchini kwani jukumu hilo ni zito na si la kufanyia utani hata kidogo,

Lundenga ameongeza kuwa kila mtu ana matatizo yake lakini kuna matatizo yanavumilika lakini mengine inakuwa vigumu kuyavumilia hivyo mrembo huyo ametakiwa kutangaza vyema utalii wa nchi yetu na utalii wake kupitia tabia yake pia.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Peter Mwenguo akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano wa bodi hiyo leo wakati alipomkabidhi zawadi zake balozi wa Utalii nchini Miss Domestic Tourism baada ya kunyakua taji hilo kwenye shindano la Vodacom Miss tanzania mwanzoni mwa mwezi huu ambapo mrembo Miriam Gerald kutoka Mwanza aliibuka mshindi, kulia ni Maria Mmari Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii na kushoto ni Hashim Lundenga Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Peter Mwenguo kushoto akimkabidhi kompyuta yenye thamani ya shilingi 1.1 Balozi wa Utalii nchini (Miss Domestic Tourism) Sia Ndaskoi katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za bodi hiyo jengo la IPS jijini Dar leo, anayeshuhudia katikati ni Maria Mmari Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii, Sia pia amekabidhiwa cheki yenye thamani ya shilingi 2.2.
Miss Domestic Tourism 2009 Sia Ndaskoi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Utalii na Kamati ya Miss Tanzania kuanzia kushoto ni Hashim Lundenga mwenyekiti kamati ya miss Tanzania, Peter Mwenguo Mkurugenzi Bodi ya Utalii, Maria Mmari Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii, Geofrey Meena Meneja masoko Bodi ya Utalii, Serena Shao Meneja wa Huduma za Utalii na Albert Makoye Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment