Rais Kikwete azindua mradi wa umeme Kilolo na kutembelea shamba la Ngo'mbe la Philips!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa umeme katika wilaya mpya ya Kilolo.Mradi huo unatekelezwa na wakala wa nishati vijijini(Rural Energy Agency) na unakadiriwa kugharimu Sh.1,665,600,000/-.(picha na Freddy Maro).

Baadhi ya wakazi wa wilaya mpya ya Kilolo wakisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwahutubia.

Muasisi wa Shamba la Mifugo la Philips Bi.Elizabeth Philips(84)(Aliyekaa kwenye wheel chair) akisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipotembelea shamba hilo kujionea ng’ombe wanaofugwa kisasa leo mchana

Mmiliki wa Shamba la mifugo la Philips Bwana Richard Philips akimuonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya ngo’mbe wa maziwa wanaofugwa kwa kutumia utaalamu wa kisayansi nje kidogo ya manispaa ya Iringa leo mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment