Rais Kikwete azindua kliniki ya meno Ilembo!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi kliniki inayotembea(Mobile Health Lab) kwaajili ya kutoa huduma za upimaji ukimwi na huduma nyinginezo za kimaabara katika uwanja wa Shule ya Msingi Ilembo, Mbeya vijijini.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya Dr.Inge Baumgarten na kulia ni afisa kutoka taasisi ya jeshi la Marekani ya Walter Reed Army Institute Bwana Edward Sekonde(picha na Freddy Maro)..
Mganga wa meno katika kliniki ya Meno kata ya Ilembo wilaya ya Mbeya vijijini Dr.Marietha Sanga akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mitambo mipya ya kuhudumia wagonjwa wa meno inavyofanyakazi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua kliniki hiyo jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wafanyakazi wa kujitolea kutoka taasisi ya American Peace Corps Meesh Santoro(wapili kushoto) anayeishi kata ya Ilembo na Jenna Covey anayeishi Isangati Mbeya vijijini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwahutubia wakazi wa kata ya Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini jana mchana
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Ilembo wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini.





You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. MBONA BENDERA YA TAIFA HAIONESHI RANGI YA BULUU KWA HADHI YAKE? RANGI HII INA TATIZO GANI? AU RANGI ZA CCM ZINAIMEZA RANGI YA MUUNGANO?

Post a Comment