MISS TOURISIM ILALA WALAMBA MILIONI 50 ZA CHICKEN HUNT!!

Mwandaaji wa Miss Tourism Ilala 2009 Amina Boka wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Savannah Lodge katika Hoteli ya City Paradise Mchana huu wakatika kampuni ya Chicken Hunt ambayo ni kampuni mama ya Savannah Lodge na Kampala Unirvesity ilipotangaza udhamini wa shilingi Milioni 50 kwa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 6 kwenye ukumbi wa Dar West Tabata jijini Dar es salaam.

Katika shindano hilo burudani zitaporomoshwa na bendi mbili tofauti katika kuleta ladha tofauti ambazo ni Diamond Musica na Extara Bongo wakati burudani nyingine italetwa na mtaalam wa nyimbo za Asili Mfalme Costa Siboka, katika picha wengine kulia ni Hamees Suba mkuu wa uhusiano Miss Tourism Tanzania, wa tatu ni Lucas Paul meneja mkuu Chicken Hunt na mwisho ni Pascal Boniventure Meneja wa Savannah Lodge nyuma ni warembo watakaoshirikia katika shindano hilo la pili kwa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya lile la Temeke kumalizika.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment