KATIBU MKUU VIWANDA NA BIASHARA AZINDUA TAMASHA LA BIASHARA!!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Joyce Mapunjo akisoma risala mbele ya waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa Tamasha la Biashara la International Shopping Festival ambalo limeanza leo kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa na litaendelea mpaka Novemba 10, tamasha hilo linashirikisha nchi 11 kutoka mashariki ya kati, Asia na Afrika Mashariki, wanaofuatia katika picha kulia ni Edwin Novath Rutageruka Director of Export Promotion (BET) na Ali Nizam General Manager Nizam Exhibitions Co.
Katibu mkuu wa Wizara ya Biashara na viwanda Joyce Mapunjo akiwa katika picha ya Pamoja na kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo linalojulikana kama International Shopping Festival.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi tamasha la biashara linalofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa.
Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Joyce Mapunjo akiwa ameongozana na Balozi wa Syria Ahmamed Mansoor wakati walipotembelea mabanda mbalimbali katika tamasha la biashara lililozinduliwa leo kwenye viwanja hivyo.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la biashara lililoanza leo kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment