
Bi Hoyce Temu akionyesha kitabu chake alichokitunga kinachoitwa Nakumbuka Yote wakati wa Uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa Jana, kitabu hiki kinahusu maisha yake na ameyaelezea maisha yake hayo kwa undani kabisa, kitabu hiki kinapatikana katika maduka mbalimbali ya vitabu hapa nchini na katika ofisi za Mkuki na Nyota Publishers na kinauzwa kwa bai ya shilingi elfu 5.000 tu kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0788-400100.

Waziri wa Jinsia wanawake watoto mama Magreth Sitta na Hoyce Temu wakiwa wameshika kitabu cha Nakumbuka Yote kilichotungwa na Hoyce Temu mwenyewe mara baada ya kuzinduliwa na waziri huyo jana kwenye Hoteli ya New Africa.

Waziri wa Jinsia wanawake na Watoto mama Magreth Sitta katikati akiingia kwenye Hoteli ya New Africa tayari kwa kuzindua kitabu kilichotungwa na Hoyce Temu kinachoitwa Nakumbuka yote wanaomsindikiza kushoto ni Hoyce Temu na kulia ni Godwin Barongo.

Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publishers ambao ndiyo wachapishaji wa kitabu hicho Bw. Walter Bugoya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar jana.

Mgeni rasmi Waziri wa Jinsia wanawake na watoto mama Magreth Sitta akiwa katika picha ya pamoja na Hoyce pamoja kushoto, mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Walter Bugoya aliyesimama kulia na ndugu zake ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa mafanikio yake mpaka hapo alipofikia.

Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Zanaki ambao wanasoma mchepuo wa Lugha ya Kiswahili wakiangalia kitabu cha Nakumbuka Yote kilichotungwa na Hoyce Temu.

Hawa ni marafiki wa Hoyce Temu kulia ni Bege Mwaimu na Fiderin Ilanga wakijadiliana jambo

Milie kutoka Mkuki na nyota Publishers ambao ndiyo waliochapisha kitabu hicho akiwa katika pozi.

Hiki ndiyo kitabu kilichotungwa na Bi. Hoyce Tema aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1999, kitabu hiki kinaelezea maisha yake kwa undani sana na kinaitwa (Nakumbuka Yote).

Aliyekuwa mshiriki wa Project Fame Carol Uliwa akipozi katika picha na Wadau kutoka TBC1 kuklia ni Jane John na kushoto ni Angela Msangi.
0 comments:
Post a Comment