YANGA YABANWA MBAVU NA WANAJESHI SHAMBA LA BIBI!!

Kikosi cha timu ya Yanga.

Timu ya Yanga imelazimishwa suluhu ya magoli 2-2 na timu ya JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani katika uwanja wa Uhuru au Shamba la Bibi kama unavyojulikana kwa sasa ikiwa ni mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom , walikuwa ni yanga ambao walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wao Kigi Makasi mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Katika kipindi cha pili JKt Ruvu waligangamala kijeshi zaidi na kujipatia magoli mawili kupitia kwa wachezaji wake Mwinyi Kazimoto na Hussein Bunu kitu kilichopelekea timu ya Yanga na mashabiki wake kuwa katika wakatii mgumu sana kutokana na ugumu wa mchezo huo
Hata hivyo katika dakika za majeruhi yanga walijitutumua na kulazimisha sare baada ya mchezaji wake huyohuyo aliyefunga goli la kwanza ambaye ni Kigi Makasi kuzifumania nyavu tena katika muda wa nyongeza na kufanya matokeo hayo kuwa sare ya 2-2 hivyo kuleta unafuu kwa mashabiki wa timu hiyo ya mtaa wa Jangwani jijini Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment