WAZIRI WA KAZI WANAWAKE NA WATOTO ZANZIBAR ALA FUTARI NA WATOTO YATIMA!!

Waziri wa Kazi, Vijana, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Asha Abdallah Juma, akimkabidhi gunia la mchele Talib Machano baada ya Madrasa yao ya Nuria kuibuka mshindi katika shindano la kuhifadhi Koran. Hafla hiyo iliyodhamini na Zain Tanzania ilifanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Bwawani Zanzibar ambapo Zain pia ilifuturisha watoto yatima. Katikati ni Mratibu wa Zain wa Kuendeleza Biashara Zanzibar, Dominick Coy na kulia ni Mkurugenzi wa Chuchu Radio, Yusuph Chuchu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Zain Zanzibar (kushoto na nguo za pink) na Waziri wa Kazi, Vijana, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Asha Abdallah Juma (hijabu ya nyano) na Mbunge wa Viti maalum, Al-Sheymaa Kwegir (hijabu nyeupe), wakifuturu pamoja na watoto yatima mjini Unguja katika futari iliyoandaliwa na Zain mwishoni mwa wiki.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment