WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL LEO.

Meneja wa kinyaji cha Redds Kabula Nshimo akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kutembelea kiwanda cha Tanzania Breweriers Limited kilichopo Ilala jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali juu ya uzalishaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kiwanda hicho,
TBL ni mdhamini mwenza wa Vodacom katika shindano hilo ambapo imedhamini kupitia kinywaji chake cha Redds na shindano hilo linatarajiwa kufanyika oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Mtaalam wa kupika bia Bw. Carvin Nkya akiwaelezea jambo warembo wa Vodacom Miss Tanzania jinsi bia zinavyopikwa katika mitambo yao.
Hapa wakielezwa nwa mtaalam wa kutengeneza bia Bw. Carvin Nkya jinsi mtambo (haupo pichani) wa kusafisha maji taka jinsi unavyofanya kazi baada ya maji hayo kutumika kiwandani hapo ili kutunza mazingira.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiingia kiwandani hapo kwa ajili ya kutembelea ili kujifunza mambo mbalimbali juu ya uzalishaji wa vinywaji mbalimbali kiwandani hapo.

Moja ya mitambo inayoinayofunga bia mara baada ya kujazwa pombe na mashine maalum kama unavyoona chupa za bia aina ya Ndovu zikiwa zikitoka kwenye mashine hiyo zikiwa tayari zimeshafungwa ikwa ajili ya kwendfa kwa mlaji.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment