MORAVIAN MBEYA MJINI KUIPUA MPYA HIVI KARIBUNI!!

Kwaya ya Moravian Mbeya Mjini iko jijini Dar es salaam kwa muda wa wiki mbili sasa ikirekodi nyimbo zake mpya kwenye studio za CVC Chan'gombe ambapo inasemekana albam yao mpya itakuwa na nyimbo 10 sawa na ile ya kwanza iliyokuwa ikiitwa :
"Bwana ndiye Mchungaji wangu" ambayo pia ilikuwa na nyimbo 10
Mmoja wa viongozi wa kwaya hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema wanatarajia kuwa albam yao itakuwa ya kufurahisha na yenye nyimbo kali sana kwakuwa hata albam yao ya kwanza ilikuwa nzuri na watu mbalimbali waliipenda, Wapendwa katika jina la yesu sisi FULLSHANGWE tunawatakia kila mafanikio kwenye kazi yenu hiyo ya kurekodi albam yenu mpya na mungu atakuwa pamoja nanyi kwani mnafanya kazi ya mungu Amin.
(Wadau kaeni mkao wa kusifu na kuabudu).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment