WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WALA RAHA KWENYE KISIWA CHA MBUDYA!!

Mrembo Suzan Emamanuel ambaye pia ni Miss Arusha akikata keki kama ishara ya Birthday yake kutimiza miaka 21, huku warembo wenzake wakiwa wamemzunguka, wakati alipofanyiwa pati ya kushitukiza kwenye kisiwa cha Mbudya leo kilichoko pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es salaam, Vodacom iliandaa tamasha hilo lililokwa mahsusi kwa ajili ya warembo kupumzika na kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa kikapu, Pete Mpira wa miguu na Kuogelea, mpaka sasa imebaki wiki moja ili shindanola Vodacom Miss Tanzania lifanyike ambapo mwaka huu litafanyika oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City mwaka huu jijini Dar es salaam huku gwiji la muziki wa Rhumba Africa Koffie Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo litakaloporomosha burudani kali kabisa katika shindano hilo.
Wachezaji wa timu ya M. Pesa wakimzonga mwamuzi kwa kuwaminya katika maamuzi yake wakati wa mchezo wao wa soka la ufukweni dhidi ya The Gread katika tamasha la michezo na burudani liliofanyika katika kisiwa cha Mbudya jijini Dar leo.
Wachezaji wa Tuimu ya M. Pesa wakishangilia mara baada ya kuwashida wenzao wa timu ya The Gread katika mchezo wa kuvuta kamba katika tamasha lililoandaliwa na Vodacom katika kisiwa cha Mbudya jijini Dar es salaam leo.
Hapa Timu ya M.Pesa na The Gread zikishindana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo timu ya M.Pesa ilishida.
Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania wakishangilia timu yao ya The Gread wakati wa timu za M. Pesa na The Gread ziliposhindana katika kucheza mpira wa wavu katika kisiwa cha Mbudya leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment