Kama unavyoona mdau jinsi ubao wa matangazo wa kituo kikuu cha shirika Reli ya kati TRL kinavyosomeka hata hivyo imeelezwa na wafanyakazi wa shirika hilo kuwa safari ya kwenda bara siku ya leo imesitishwa kutokana na mwajiri wao kuchelewesha mishahara yao ya mwezi uliopita, hivyo wameona hakuna njia ya kufanya ili kupata mishahara yao ila ni kusitisha huduma hiyo.
Wafanyakazi hao wameongeza kuwa imekuwa ni kawaida kila inapofika wakati wa kulipwa mishahara hiyo, kunakuwa na visingizio vingi vya kuchelewesha mishahara yao bila kujua kuwa na wao wana famila zao ambazo zinawategemea majumbani mwao.
Wameongeza kuwa tayari wamechukua hatua ambapo wameutuma uongozi wao wa TRAWU wa kanda na wajumbe wake ili kufuatilia suala hilo "sisi tuamhitaji waziri wa Miundo Mbinu Shukuru Kawambwa , Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda na huo uongozi wa TRL ili tujue hatima yetu kwani tunapata matatizo mengi ambayo yanahitajika kutatuliwa, bila kujua hatima ya mishahara yetu hakutakuwa na huduma ya usafiri na katika hili wananchi ama abiria ndiyo wanaoathirika zaidi" .
Hali ndiyo iko hivyo wasafiri wamekwama katika kituo kikuu cha leli ya kati TRL jijini Dar es salaam kutokana na wafanyakzazi wa shirika kusitisha huduma kwa madai ya kutolipwa mishahara yao ya mwezi uliopita.
Hawa wakionekana kuchoka kutokana na kupewa taarifa kuwa treni ya kwenda iliyokuwa iondoke kwenda bara haitaondoka kutokana na wafanyakazi kusitisha huduma kwa madai ya kuchelewesha mishahara yao ya mwezi uliopita wa Agosti.
1 comments:
Bongo tambalare mimi yangu macho.
Post a Comment