VODACOM KUTUMIA MILIONI 17 MASHINDANO YA BAISKELI MWANZA!!

Meneja matukio wa Vodacom Rukia Mtingwa kulia akizungumza na wanahabari leo kati ni mwenyekiti wa chama cha baiskeli Tanzania Addo Mapunda kushoto ni afisa kutoka kampuni ya Pepsi.

Meneja matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa leo ametangaza zawadi za washindi watakaopatikana katika mashindano ya baiskeli yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza mwezi ujao,
Rukia amesema Vodacom imetenga jumla ya shilingi milioni 17 ili kufanikisha mashindano hayo kama zawadi kwa washindi mbalimbali watakaoibuka washindi katika mashindano hayo, vodacom imekuwa ikiandaa mashindano hayo kwa mwaka wa nne mfurulizo na mwaka huu wameboresha kwa kiwango kikubwa kwa upande wa zawadi ambapo washindi wanatarajiwa kuondoka na zawadi nono.
Rukia amesema mashindano hayo mwaka huu yamegawanyika katika makundi 4 ambapo kundi la kwanza ni la mbio za km 150, kundi la pili km 80 wanawake na kundi la mwisho ni la km 10 ambalo litahusisha walemavu.
Akitaja zawadi hizo amesema mshindi wa mbio za km 150 atapata shilingi 1.200.000 wakati mshindi wa pili atapata shilingi 900.000 na mshindi wa tatu atapata shilingi 600.000 mshindi wa 4 hadi wa 10 atazawadiwa shilingi 450.000 wa 11 mpaka 20 200.000 kila mmoja na wa 21 mpaka 30 ataondoka na kitita cha shilingi 100.000.
Kwa upande wa mbio za km80 mshindi wa kwanza ataondoka na shilingi 1,000.000 mshindi wa pili shilingi 750.000 mshindi wa tatu 500.000 mshindi wa 4 mpaka wa 10 watapata shilingi 320.000 mshindi wa 11 mpaka 20 watapata shilingi 120.000 na wa 21 mpaka 30 watapata shilingi 60.000 kila mmoja.
Kwa upande wa kundi la walemavu wanawake na wanaume mshindi wa kwanza atapata shilingi 300.000 mshindi wa pili atapata shilingi 200.000 washindi wa tatu kila mmoja atapokea shilingi 100.000 na kuanzia mshindi wa 4 mpaka wa 10 watapata shilingi 50.00 kila mmoja wakazi wa mwanza wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mbio hizo wakata burudani itatolewa na TMK wanaume Family na Tiptop Connection

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment