TBL yatoa msaada wa stika na fulana Wiki ya Nenda kwa Usalama!!

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyoafanyika Dar es Salaam jana, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu akibandika stika kwenye gari Dar es Salaam jana, yenye maneno yanayotahadharisha madereva kutoendesha magari huku wakiwa wamelewa. Stika hiyo ni moja kati ya 4000 zilzotolewa msaada na TBL kwa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama, Dar es Salaam jana. Pia TBL ilitoa msaada wa fulana 800 kwa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe,


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment