Jaji Mkuu wa Tanzania na Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini TBF Jaji Augustino Ramadhan akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo asubuhi wakati alipotangaza maandalizi ya bonaza la mpira wa kikapu lililopewa jina la "BASKETBALL CHARITY DAY" litakalofanyika kuanzia oktoba 17 mpaka 22 na kuhitimishwa tarehe 24 kwa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa viwanja zaidi ya vitano nchini kote huku mgeni rasmi akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete, jumla ya shiligi milioni 10 zinatarajiwa kukusanywa katika Harambee hiyo , wanaofuata katika pisha ni Lawrence Cheyo Katibu mkuu wa TBF na Saimon Msofe Mwenyekiti wa caha cha Basketball jijini Dar es salaam (DABA).
Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF Lawrence Cheyo akimkaribisha Mlezi wa shirikisho hilo Jaji mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhan wa pili kutoka kulia wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar, anayefuatia ni Eke Mwaipopo mchezaji wa zamani mpira wa kikapu na mwenyekiti wa kamati ya tamasha la kikapu linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

0 comments:
Post a Comment