
Kocha wa Timu ya Simba ya Mtaa wa Msimbazi mzambia Patrick Phiri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mpira kumalizika kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom iliyoendelea leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo timu ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa magoli 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera,
Simba ilipata magoli yake kupitia kwa wachezaji wake Haruna Moshi (Boban) katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo na katika kipindi cha pili mchezaji wake aliyetokea benchi Mohamed Kijuso aliandika goli la pili kwa upande wa Simba hivyo kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa 2-0
Hata hivyo Afisa Habari wa timu hiyo Cliford Ndimbo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo amesema mwamuzi wa mchezo huo ameshindwa kuumudu pamoja na kwamba hakuipendelea simba wala Kagera Sugar, lakini maamuzi yake hayakueleweka mara nyingi na alipoulizwa juu ya watani wao Yanga ambao wamekuwa wakisuasua katika michezo yake alijibu kuwa "kwakweli hali ni TETE kwa wenzetu"

Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Mlage Kabange akiwakimbia waandishi wa habari baada ya kukataa kuongea nao baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa wekundu wa msimbazi Simba katika shamba la Bibi yaani uwanja wa Uhuru.

Wacgezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kuandika goli la pili kupitia kwa mchezaji wake Muhamed Kijuso aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kilichopepetana na Simba Jioni ya leo na kuangukia pua.

Kikosi cha Simba Sports Club kikpozo kwa picha kabla ya mtanange hu uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment