Akizungumza mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya habari maelezo, Mrisho Mpoto amesema ametunga nyimbo tatu ambazo zitakuwa mahsusi kwa ajili ya maadhimisho haoy kutokana na ujumbe uliomo katika nyimbo hizo
Mpoto amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Mtatuua, Tuzungumze na Inawezekana ambazo zote kwa pamoja zinahamasisha watu wote wanaoutumia vyombo mbalimbali vya usafiri na waenda kwa miguu kutumia vyema barabara huku wakiachana kabisa kutuzitumia barabara hizo wakiwa wamelewa.
Mwaka juzi kamati ya usalama barabarani kanda maalum liliitumia bendi ya Akudo Ipackt katika kuadhimisha wiki hiyo, na mwaka jana waliitumia bendi ya Msondo (baba ya muziki) ndiyo iliyotumbuiza katika maadhimisho hayoa, kimzungumzia msanii Mrisho Mpoto katibu mkuu wa kamati ya usalama barabarani ACP Vitus Nikata amesema mwaka huu wameamua kumtumia Mpoto katika maadhimisho hayo kutokana na ujumbe uliomo katika nyimbo zake na jinsi anavyokubalika na jamii katika uimbaji wake
Waliopo katika picha kutoka kulia ni ACP wa polisi Vitus Nikata na katibu wa kamati ya usalama barabarani, Dosh Shoto mjumbe wa kamati hiyo , msanii Mrisho Mpoto, S/SGT Swaleh Telaki na mwisho ni Mrakibu mwandamizi wa polisi (RTO) Kinondoni na kaimu katibu wa kamati ya usalama barabarani Fortunatus Musilimu.





0 comments:
Post a Comment