BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ!!

Habari zilizotufikia hivi karibuni zinasema huko Mbagala kuu Bomu limeripuka na kuuwa watu wawili na kujeruhi watu wengine kwa, mujibu wa habari kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mbagala kuu aliyefahamika kwa jina moja la mwinde amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na inasemekana kwa sasa viongozi mbalimbali wanaelekea eneo la tukio ili kujua hasa kinachoendelea baada ya tukio hilo.
Hata hivyo bado jeshi la polisi halijatoa taarifa yoyote kwa sasa kufuatia tukio hilo na FULLSHANGWE inaendelea kufuatilia ili uwapa taarifa zaidi baadae hapo awali katika kambi ya jeshi wananchi JWTZ mbagali yalilipuka mabomu na kusababisha vifo na kujeruhi watu kadhaa huku milipuko hiyo ikiharibu nyumba za wakazi wa eneo hilo wanaoisha karibu na kambi hiyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment